Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mafuriko Yaathiri Masomo Kwa Wanafunzi Milioni 10 Katika Nchi 4 Za Afrika Magharibi na Kati.

Chanzo: Dw

Takriban watoto milioni 10 katika nchi nne za magharibi na kati mwa Afrika wanashindwa kuhudhuria masomo shuleni kutokana na mafuriko makubwa ya kikanda.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Save the Children imesema mafuriko nchini Nigeria, Mali, Niger na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha takriban watu milioni moja kuyahama makazi yao.


Pia Shirika hilo limesema kuwa mvua ambazo hazijawahi kushuhudiwa, zimesababisha mzozo unaozidi kuwa mbaya wa elimu baada ya kuharibiwa kwa shule, pamoja na majengo ya shule kutumiwa kama makazi ya muda kwa waliopoteza makazi yao na kuhama kwa familia kutoka maeneo ya karibu na shule.


Hata hivyo shirika la Save the Children, imetoa wito kwa serikali kupanga haraka mikakati mbadala ya watoto wanaokosa masomo na kuhakikisha kuwa shule zinawekwa katika hali ya kustahimili zaidi hali mbaya ya hewa katika siku zijazo huku likiwataka wafadhili wake kuongeza msaada kwa watu walioathirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *