MAENDELEO HAYAJI HIVI HIVI NI LAZIMA KUTIMIZA WAJIBU – RC BALOZI SIRRO

NA FAUSTINE KASALA, KIGOMA .

Watumishi wa Idara za Serikali Taasisi na vitengo mbalimbali manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kutumia taaluma zao kuisaidia jamii kujiletea maendeleo kwa lengo la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja mkoa na hata Taifa kwa ujumla

Akizungumza na wakuu wa Idara taasisi na wawakilishi wa makundi mbalimbali katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha  Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Nyakolo Sirro amesema adhima ya Serikali kuwaweka katika vitengo walivyo navyo ni kuisaidia jamii   kuondokana na hali duni ya maisha

”Niwaambie maendeleo hayaji hivi hivi bila juhudi za watu ambao wanatakiwa kufanyiwa maendeleo na wanaopaswa kufanya hivyo wasipotimiza wajibu wao, wataalam wote mlioko hapa mmefanya nini kuwasaidia wafugaji wakulima wafanyabiashara ili kufikia adhima ya ufugaji ama Kilimo chenye tija, mmefanya nini!’’ Alisema Balozi Sirro.

Aidha Balozi Sirro amesisitiza suala la uwekezaji na kukuza utalii katika mkoa huo kwa kuzingatia kilimo Biashara.

Awali akitoa salaam kwa mkuu wa mkoa mkuu wa wilaya ya Kigoma Dr Rashidi Chuachua amesema Manispaa ya Kigoma Ujiji Tangu Rais Samia aingie Madarakani zaidi ya billion 14 Zimepokelewa katika Manispaa hiyo na kuelekezwa katika miradi ya Afya, Utawala kilimo mifugo Biashara na uwekezaji.

”Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Halmashauri yetu ya Kigoma iko salama  sana na watumishi wake wote wanafanya kazi kwa kujituma ili kufikia malengo ambayo Serikali imejiwekea Tangu Rais Samia aingie Madarakani Manispaa ya Kigoma Ujiji imepokea zaidi ya Trilion 7 ambazo zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya miundo binu kama vile ujenzi wa Barabara Meli nk.” Alisema Dr Rashidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya kilimo Mifugo na Uvuvi Adam Moshiro amesema wanaendelea kutoa elimu kwa vikundi mbalimbali vya ufugaji na kilimo ili viweze kuondokana na ufugaji na kilimo cha mazoea kisicho kuwa na tija sambamba na kuwasaidia namna ya kupata masoko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *