Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema hadi kufikia mwezi huu wa Februari 2025, jumla ya Wanajeshi 46,000 wameuawa na makumi ya maelfu hawajulikani walipo tangu kuanza kwa vita februari 2022.
Zelensky ameyasema hayo katika mahojiano huko Kyiv ambapo amedai kuwa Wanajeshi wasiojulikana walipo, huenda walikufa au bado wanashikiliwa mateka na vikosi pinzani.

Kaauli ya Zelensky inakuja wakati huu ambapo Ukraine imetengwa kwenye mazungumzo ya amani, kati ya Marekani na Urusi ingawa awali alisema hakujumuishwa na hatatambua mapatano yaliyoafikiwa bila kushirikishwa.