Maduka zaidi ya 900 yaliteketea

Moto mkubwa ulioibuka jumapili (Oktoba 1,2023) katika eneo la Big Bon, Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuteketeza maduka takribani 1,000 yakiwamo ya vifaa vya magari yaliyo chini ya Kampuni ya Kariakoo Auction Mart na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.

Moto huo ulianza majira ya saa 12.30 asubuhi katika maduka ya kampuni hiyo na kusambaa hadi kwenye majengo jirani.

Baadhi ya wafanyabiashara walifanya jitihada za kuzima moto huo baada ya Jeshi la Zimamoto kufika eneo la tukio wakiwa hawana maji.

Moto huo umeteketeza mali huku madirisha, matangi ya maji na nyaya za umeme za maghorofa ya jirani nazo zikiharibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *