Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Madiwani watakiwa kuhakiki kampuni za ulinzi ili kubaini wahalifu- Geita

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limewataka Madiwani wote katika Halmashauri za Mkoa huo kuhakiki kampuni zote za ulinzi zilizopo katika maeneo yao kwa lengo la kubaini uwepo wa walinzi wasio waaminifu na ambao wamekuwa wakitumia mwanya wa ulinzi kufanya matukio ya uhalifu hali ambayo imekuwa ikichochea matukio hayo kuongezeka kila kukicha.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Safia Jongo wakati akizungumza katika kikao maalumu cha baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG ambapo amesema walinzi wamekuwa wakishirikiana na majambazi kufanya uhalifu kutokana na kampuni hizo kutosajiliwa katika maeneo husika.

Aidha Kamanda Jongo ametumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kushirikiana na viongozi wa mitaa na vijiji katika maeno yao kuanzisha madaftari ya kudumu ya wakazi na wageni ili kubaini wahalifu kwa uraisi zaidi katika maeneo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *