Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga limelaani vikali vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia katika wilaya hiyo kutokana na kukithiri matukio ya mara kwa mara yanayosababisha mmomonyoko wa maadili hasa ukatili wa kijinsia kwa watoto hususani ulawiti na ubakaji pamoja na mahusiano wa jinsia moja.
Baraza hilo la madiwani lililokuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Amani Juma Kasinya limetoa tamko hilo lilipokaa katika kikao cha robo ya pili cha mwaka wa fedha 2023/2024 na kuziagiza mamlaka zinazoshughulikia kesi hizo kutoa adhabu kali kwa wote watakaothibitika kutenda vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa wengine