Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Madiwani na Tanesco mshirikiane

Madiwani wanaounda Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuainisha maeneo ya vipaumbele katika kata zao wakati wa utekelezwaji wa zoezi la usambazaji wa nishati ya umeme ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zitokanazo na ukosefu wa nishati hiyo katika maeneo hayo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi kupitia kikao kazi cha Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO mkoa wa Shinyanga na madiwani wa Manispaa hiyo na kuagiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili ili kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe amebainisha vipaumbele katika kufikisha huduma ya umeme kwa wananchi huku meneja mradi wa REA kutoka Suma JKT akianisha hatua zilizofikiwa katika utekelezaji mradi wa kusambaza umeme kwa wananchi katika vijiji saba vya Manispaa ya Shinyanga.

Kikao hicho chenye kauli mbiu ‘TANESCO Yetu, Umeme Wetu, Njoo Tuzungumze’ kimekwenda sambamba na utoaji wa taarifa ya hali ya maendeleo ya Mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na Maendeleo ya Mradi wa umeme jua unaotekelezwa katika kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *