Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu leo Februari 9, 2024 limewakutanisha na kuwapa elimu madereva wa magari ya serikali mkoani humo kwa lengo la kuwajengea uelewa zaidi kuhusu sheria za usalama barabarani.
Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa madereva hao wa serikali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe amelitaja lengo la mafunzo hayo kuwa ni kupunguza ajali za barabarani sambamba na kuepuka ukiukwaji wa sheria.
Aidha, ACP. Swebe amewakata madereva hao kuzingatia mafunzo hayo ili yawe chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi wao na kuzingatia sheria za usalama barabarani.