‘MADEREVA KUWENI MAKINI NA WAANGALIFU BARABARANI’ – RAIS SAMIA..

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka madereva wote kuendelea kuwa makini na waangalifu zaidi barabani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Rais Samia ameyasema hayo kwenye chapisho lake kwenye mitandao ya Kijamii akitoa pole kwa wafiwa na majeruhi wa ajali iliyotokea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Rais Samia ameandika ‘Nimesikitishwa na taarifa ya vifo vya ndugu zetu 9 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya kutoka Tarekea, Wilaya ya Rombo kuelekea mji wa Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro. Ninawaombea marehemu wapumzike kwa amani. Ninatoa salamu za pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa, na ninawaombea majeruhi wapate nafuu kwa haraka’. – Rais Samia

‘Nasisitiza madereva kuendelea kuwa makini na waangalifu zaidi barabarani, huku Jeshi la Polisi likiendelea na kazi ya kusimamia sheria za usalama barabarani wakati huu wa mwisho wa mwaka’. – Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *