MADAWATI USTAWI WA JAMII SASA KUPATIKANA KATIKA VITUO VYA MABASI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni amewataka wakurugenzi kutoka katika halimashauri za Manispaa ya Shinyanga na Kahama kuhakikisha wanatenga vyuma maalum vitakavyotumika kama ofisi za dawati la jinsia katika stendi zao za mabasi ili kunusuru usalama wa watoto wanaoishi kwa kufanya kazi mitaani.

CP Hamduni ametoa maagizo hayo hii leo February 11 2025 wakati akifungua kikao cha  uanzishwaji wa dawati la ustawi wa jamii katika Kituo Kikuu cha Mabasi Manyoni kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  pamoja na Kahama kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, mradi ambao unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika la Railway Children Afrika (RCA).

Ameipongeza ofisi ya rais-TAMISEMI kwa kuleata mradi huu katika mkoa wa Shinyanga pamoja na mikoa mingine kumi  kunakotekelezwa mradi huo, huku akiweka wazi kuwa Shinyanga ni moja ya mikoa yenye changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani jambo ambalo limekithiri aidi katika Halmashari ya Manispaa ya Kahama.

“Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imekuwa ikipokea watoto wanaotoka nchi jirani ya Burundi  na changamoto hii imepelekea watoto hawa kujifunza na kujiingiza katika tabia hatarishi na wakati mwingine kutumwa na watu wazima kufanya matukio ya wizi,uporaji,biashara ya ngono,na matumizi ya dawa kulevya,” amesema CP Hamduni.

Ameanisha jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika kupitia Halmashauri na Idara ya Uhamiaji na Polisi kuwa  ni kuwabaini watoto hao kwa  kuwafanyia tathmini,na kuwahifadhi sehemu salama na kisha kuwaunganisha na familia zao. Aidha watoto baadhi ya watoto ambao wamekuwa wakirudi licha ya kurejeshwa.

Hamduni amesema, “kupitia mradi huu ni Imani yangu utasidia kuja na mikakati madhubuti ya kuondokana na changamoto hii na kuwa na uendelevu wa dawati hili hata kama mradi utakuwa umeisha kwani ni jukumu la Seikali kuona ipo haja ya kuimarisha mashirikiano kwa Serikali, Taaisisi mbalimbali, jamii na walezi katika kuhakikisha tunadhibiti watoto hawa kutoingia mtaani kwa kuimarisha malezi na makuzi.”

Aidha, amesema ni wajibu wa wazazi na walezi kuimarisha uchumi wa familia na  mifumo ya ulinzi wa watoto kwani uanzishwaji wa dawati la ustawi katika Vituo vya mabasi utasaidia kuweza kuwabaini watoto mapema mara tu wanaposhuka na mabasi, kuzuia kuingia mitaani na  kuweza kubaini mahitaji  yao

Naye Meneja Utekelezaji wa Miradi kutoka Shirika la Railway Children Afrika ambalo limeingia ubia na Serikali kupitia TAMISEMI kutekeleza mradi huo, Dionis Shimbi amesema watatumia fura ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kuimarisha ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na kutambua na kutatua changamoto za watoto wote wanaofanya kazi za mitaani.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga, Lyidia Kwesigabo amesema mkoa utatekeleza mradi huo kwa kuzingatia sheria ya mtoto na 21 ya mwaka 2019 pamoja  na kanuni ya  usalama wa mtoto katika kuwahudumia watoto wote watakaobanika kuishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwaptia huduma na hatimae kuwaunganisha tena na familia zao.

One response to “MADAWATI USTAWI WA JAMII SASA KUPATIKANA KATIKA VITUO VYA MABASI”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *