Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga, Christina Solomon Mndeme Amezitaka Halmashauri Zote Ndani Ya Mkoa Wa Shinyanga Kukamilisha Ujenzi Wa Miradi Ya Boost Kabla Ya Tarehe 10 Julai, 2023 Ili Wananfunzi Waweze Kuanza Kunufaika Na Miundombinu Hiyo.
Mndeme Ameyasema Hayo Alipokuwa Akikagua Ujenzi Wa Madarasa Matatu (3) Na Matundu Ya Vyoo (3) Katika Shule Ya Msingi Busongo Iliyoka Halmashauri Ya Msalala Na Shule Mpya Yenye Jumla Ya Madarasa 16 Inayojengwa Manispaa Ya Kahama Ambayo Alipendekeza Iitwe SHULE YA MSINGI ANDERSON Ikiwa Ni Sehemu Ya Kutambua Mchango Wake Mkubwa Katika Utekelezaji Wa Miradi Ya Maendeleo Manispaa Ya Kahama Huku Akiwaagiza Viongozi Wa Kamati Za Shule Na Wananchi Kuitunza Miradi Hiyo.
Mkoa Wa Shinyanga Pamoja Na Mambo Mengine, Kwenye Sekta Ya Elimu Inajenga Shule Za Msingi 9 Mpya, Madarasa 84 Na Matundu Ya Vyoo 133 Ikiwa Ni Sehemu Ya Utekelezaji Wa Mradi Wa Boost.