MADARAJA MATATU YAMFIKISHA SILLO ENDABERG

Na Saulo Steven – Manyara.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo, amekagua maendeleo ya ujenzi wa madaraja matatu yanayoendelea kujengwa katika Kijiji cha Endaberg, Kata ya Riroda, Wilaya ya Babati.

Ujenzi wa madaraja hayo unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha miundombinu ya usafiri na mawasiliano katika Jimbo la Babati Vijijini.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Sillo ameipongeza Serikali kwa uwekezaji huo mkubwa ambao utasaidia kurahisisha usafiri kwa wakazi wa eneo hilo, hususan wakulima na wafanyabiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *