MADAI YA KUCHAPISHA FEDHA ZA UCHAGUZI: BOT WAKATA MZIZI WA FITNA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu kuwa inachapisha na kusambaza fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu, huku zingine zikihamasisha wananchi kuondoa fedha zao kwenye benki kwa madai baadhi ya benki zimeishiwa fedha.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba,imeeleza kuwa BoT huchapisha fedha kwa mujibu wa Kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu, Sura ya 197, na kuziingiza kwenye mzunguko kulingana na shughuli za kiuchumi na mahitaji ya kubadilisha fedha chakavu, na siyo vinginevyo.

Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, “benki zote zilizopo nchini zinasimamiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na vigezo vya kimataifa ambapo zimeendelea kuwa na mahitaji ya kutosha, ukwasi wa kutosha, zinatengeneza faida, na zina kiwango kidogo cha mikopo chechefu (asilimia 3.3 Septemba 2025) ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 5.0.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *