Wafugaji wa Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo ndani na nje ya Mkoa wa Pwani, wamepata mkombozi wa soko la uhakika la kuuza Mifugo hiyo kufuatia kufunguliwa machinjio ya kisasa ya Union Meat Group katika Kijiji cha Kwa Zoka Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Machinjio hayo, Mariam Ngh’wani aliyoitoa April 10,2025 kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Ismal Ussi amesema kutokana na uhitaji mkubwa ulipo wanaihakika wa kununua mifugo kwa wingi kutoka kwa wafugaji.

“Masoko ya nyama tunauza ndani na nje ya nchi na ni ya uhakika hivyo wafugaji wanakaribishwa kuleta mifugo hapa ili kuuza” amesema.
Ameongeza kuwa mbali na fursa za soko Kwa wafugaji pia machinjio hiyo inafanyakazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za nchi ikiwemo kutoa ajira kwa wananchi na kulipa kodi zote zinazostahili.

“Hii machinjio inafanyakazi kwa kuzingatia weledi na usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha nyama zinazotoka hapa zinakuwa na ubora wa kitaifa na kimataifa”amesema.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail Ussi amesema kuwa serikali inawajli wawekezaji kwakuwa wanamchango mkubwa wa maendeleo.

“Serikali inayoongozwa na Rais mama Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwa kutambua kuwa wanamchango mkubwa wa maendeleo nchini,” amesema.
Mkazi wa Vigwaza, Anna Mwalekwa amesema kuwa uwepo wa viwanda nchini unsaidia kukuza uchumi kwa jamii hasa kwakuongeza ajira.

Amesema kuwa mbali na ongezeko la ajira pia uwekezaji unachangia kuoanuka kwa miji na kuleta mvuto kwa wageni wanaoingia Kutoka nje na ndani ya nchi.
“Mfano mzuri wa hill jengo kiukweli linavutia sana na limebadilisha mazingira kwa muonekano wake ulivyo,” amesema.