Na Melkizedeck Antony,Mwanza
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Seleman Jafo amesema maboresho yaliyofanyika katika taasisi mbalimbali za umma nchini yamesaidia kuongezeka kwa kampuni pamoja na biashara zinazoendelea kusajiliwa ikiwa hadi Septemba 10, 2024 biashara zaidi ya 250,000 zimesajiliwa nchi nzima.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo Septemba 10,2024 wakati akifungua maonesho ya 19 ya Biashara Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza.
“Niwapongeze Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kwani licha ya kusajili bishara hizo tayari mmesajili majina ya biashara zaidi ya 551,000 hii yote tunaongeza vijana kwenye soko la ajira katika sekta binafsi msikae chini bali endeleeni kuongeza juhudi katika kurahisisha mifumo na taratibu za usajili ili wazidi kuongezeka,” alisema Dk. Jafo
Aidha alisema hatua hiyo imesababishwa na mabadiliko ya mfumo yaliyofanywa katika usajili kutoka kusajili kwa zaidi ya miezi mitatau na kusajili biashara na majina ndani ya siku tatu aidhaamesema usajili huo unaozidi kuongezeka ni ishara ya maboresho katika taasisi zote za umma pamoja na kupuzwa kwa mirorongo miresfu katika ufuatiliaji.
“Sasa hata hawa vijana na vikundi vya burudani nanyi jitahidini mkasajili majina yenu ili kulinda bunifu zenu watu wengine wasije wakaziiba,”alisema Jafo
Aidha alizitaka taasisi za biashara zote nchini kuhama katika utamaduni wa kukwamisha wafanyabiashara katika kufanikiwa kwenye shughuli zao bali ziwe msatari wa mbele kuwasaidia ili kufikia malengo yao.
“Kuna muda taasisi zetu hizi ambazo zimepewa dhamana ya kusimamia na kuwasaidia wafanyabiashara kuchukua muda mrefu zikitafuta vifungu vya sheria kwaajili ya kuwabana wafanyabiashara lakini hiyo siyo dhamira ya serikali bali tunahitaji kuweka mianya rafiki kwa wafanyabiashara ili kuwapa fursa ya kuendelea kuwekeza nchini,”alisema
Akizungumza kuhusu hali ya usajili wa Leseni Ofisa Biashara kutoka Brela Sweetness Madata alisema Wakala huo umeendelea kusajili kwa njia rahisi ambako katika maonesho hayo wanasajili papo kwa papo.