MABELE ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUZINI NA MWANAYE

Na Saada Almasi – Simiyu.

Mahakama Wilayani Maswa mkoani Simiyu imemhukumu kwenda jela miaka 30 sambamba na faini ya laki mbili Daudi Mussa Mabele maarufu kwa jina la Lesha (38) mkazi wa kijiji cha Kakola kata ya Shishiyu Wilayani Maswa kwa kosa la kuzini na maharimu wake (mtoto wa kumzaa) mwenye umri wa miaka 14 na kumpatia ujauzito.

Mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya maswa Aziz Khamis mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya Taifa ya mashtaka wilayani hapo mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Vedastus Wajanga amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo siku ya mwezi Septemba mwaka 2024 katika kijiji cha Kakola kata ya Shishiyu wilayani hapo.

Wajanga ameongeza kuwa mshtakiwa alizini na maharimu wake ambaye ni mtoto wake wa kumzaa (14) na kumsababishia ujauzito kitendo kilichotokea baada ya mama mzazi yaani mkewe kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya kujifungua.

Wajanga amesema kuwa taarifa zilifika kituo cha polisi wilaya ya Maswa na baada ya hapo mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na kuambatana na mashahidi watano waliofikishwa kutoka upande wa mashtaka pamoja na kielelezo kimoja.

Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kutendeka kwa kosa hilo baada ya ushahidi huo kutolewa mshtakiwa alipewa nafasi ya kuwasilisha utetezi wake ambapo alikiri moja kwa moja kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani ni kosa lake la kwanza na anategemewa na familia.

Mara baada ya utetezi huo kukamilika mahakama hiyo ilimtia hatiani mshtakiwa Daudi Mussa Mabele ama kwa jina lingine lesha huku mwendesha mashtaka aliimba mahakama kumpatia adhabu kali ili iwe funzo kwa wengine ukizingatia kwamba tendo hilo ni kinyume cha sheria na maadili ya mtanzania na kimeacha alama isiyoweza kufutika kwani ni ukatili wa kijinsia.

Na baada ya hapo hukumu hiyo ya kesi ya jinai yenye namba 6929 / 2025 ikatolewa hukumu na hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo Azizi Khamis kwa kutoa adhabu ya kwenda jela miaka 30 Daudi Mussa Mabele sambamba na kulipa faini ya shilingi laki mbili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *