Mabasi 314 yapewa vibali safari za usiku

Mamlaka Ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) Imeyapa Mabasi 314 Vibali Vya Ratiba Ya Kuanza Safari Za Kwenda Mikoani Kuanzia Saa 9:00 Usiku Hadi 11:00 Alfajiri.

Katika Ya Mabasi Hayo, Tisa Yameondolewa Katika Ratiba Hizo Juzi Baada Ya Kukiuka Kanuni, Sheria Na Taratibu Za Uendeshaji Na Usalama Barabarani Kwa Kuendeshwa Mwendo Kasi Kwa Lengo La Kufanya Mashindano Ya Kuwahi Kufika Kwenye Vituo Vya Mabasi.

Kaimu Mkuu Wa Kitengo Cha Uhusiano Na Mawasiliano Latra, Salum Pazzy Amesema Tangu Watangaze Ratiba Mpya Ya Mabasi Yanayotaka Kuanza Safari Saa 9:00 Usiku Na Saa 11:00 Alfajiri Desemba Mwaka Jana Hadi Sasa, Jumla La Mabasi 314 Yamepewa Nafasi Hiyo.

Mapema wiki hii , Mkurugenzi Mkuu Wa Latra, Habibu Suluo Alitoa Taarifa Ya Kuyafungia Mabasi Tisa Kuanza Safari Zake Saa 9:00 Alfajiri Na Badala Yake Yatakuwa Yanaanza Safari Saa 12:00 Asubuhi Kwa Kuwa Yamekiuka Masharti Na Kanuni Za Usafiri.

Alisema Latra Ina Jukumu La Kutoa, Kuhuisha Na Kufuta Vibali Na Leseni Za Usafirishaji Na Kukuza Usalama Wa Sekta Zinazodhibitiwa Ikiwa Ni Pamoja Na Usalama Wa Watumiaji Wa Huduma Za Sekta Zinazodhibitiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *