Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mabasi 19 yamepigwa marufuku

Mabasi 19 yanayosafirisha abiria ndani na nje ya Mkoa wa Geita yamepigwa marufuku kufanya safari za kubeba abiria kutokana na magari hayo kugundulika yana hitilafu huku mengine yakimaliza muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Geita Aloyce Jacob amesema hayo wakati wa oparesheni ya kushtukiza katika stendi kuu ya mabasi ya Mkoa wa Geita ambapo jumla ya magari 213 yamekaguliwa huku 142 yakikutwa na makosa mbalimbali.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo amesema oparesheni hiyo itakuwa endelevu kwa vyombo vyote huku akisema tayari wameanza pia ukaguzi kwa Madereva bodaboda wanaobeba abiria zaidi ya mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *