Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

“Mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria”

Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Na uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu.”“Kuhusu majeruhi Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu.”

“Tusahau yaliyopita na tuangalie mbele. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa tukipoteza na tukiwa nyumbani hatutakuwa kwenye sehemu nzuri ya kwenda hatua ya mbele. Twendeni tukawape moyo wachezaji wetu kwamba tunaanguka pamoja na kusimama pamoja.”- Ahmed Ally. 

Akaongeza “Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi. Wakati ujao wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena. Mwiba unatokea ulipoingilia.”


“Safari hii tunakwenda kuwashangaza watu, tutaujaza uwanja wa Mkapa. Niwambie Wanasimba kama una hasira uje nazo furaha utaikuta uwanjani,” amesisitiza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *