Ujumbe wa Kanisa Katoliki na Kanisa la Protestante katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), unaendelea na mashauriano yake ikiwa ni sehemu ya mkataba wa kijamii wa amani.
Madehebu hayo makuu ya DRC, mbali na kuhangaikia mapatano ya mzozo wa eneo la mashariki mwa Taifa hilo, pia wamesema wanataka kuona amani inakuwepo katika maziwa makuu.

Wanasema, mara baada ya kukutana na Mratibu wa AFC/M23 Mjini goma wameelekea jijini Kigali nchini Rwanda kukutana na Rais Paul wa Taifa hilo, Paul Kagame.
Lengo la kumuona Kagame, ni sehemu ya mkutano wao wa mashauriano ya Mkataba wa Kijamii kwa ajili ya amani na kuishi vizuri kwa amani nchini DRC.