Mwigizaji wa filamu kutoka Nigeria, Iyabo Ojo ametangaza maandamano katika mji wa Lagos kudai haki kwa marehemu Mohbad.
Iyabo alitoa tangazo hilo katika kipindi cha moja kwa moja cha Instagram siku ya Jumatatu (Leo) akisema shirika lake lisilo la kiserikali, Pinkies Foundation, litawasilisha barua kwa serikali ya eneo lake hilo la Lagos leo kabla ya mkutano wa hadhara ambapo utafanyika Jumanne au Jumatano utakaokuwa na lengo la kutaka kupatikana haki kwa msanii huyo aliyefariki wiki iliyopita ambapo kifo chake kimekuwa na maswali mengi.