Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Jijini Dar es Salaam, imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu hadi Julai Mosi, 2025 kwa ajili ya kutoa maamuzi juu ya usikilizwaji wa Kesi hiyo.
Hata hivyo, kutokana na changamoto kadhaa ambazo Mshtakiwa amesema anakabiliana nazo akiwa mahabusu, leo Juni 16, 2025 ameliomba jopo la Mawakili wa Utetezi zaidi ya 30, aweze kujitetea mwenyewe.

Hatua hiyo inakuja baada ya Tundu Lissu kudai hakuwahi kupata nafasi ya faragha ya kuongea na Mawakili wake.