Mwarobaini:
Ni mti maarufu rafiki wa binadamu, unaoaminika kuwa na asili ya Taifa la India, lakini baadaye taratibu ukaenea katika sehemu nyingi za Dunia, ikiwemo bara la Afrika.
Mti huu hutumika kutibu kwa karne nyingi na hata katika matumizi ya viwandani kutengeneza dawa, vipodozi na sabuni, huku ikiarifiwa kuwa karibu kila sehemu ya mmea huu yaani mizizi, magome, matawi, majani, maua na mbegu vyote ni dawa.
Watabibu wa kiasili wanasema Mwarobaini hutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo shida za moyo na majani ya mti huu yanapotumbukizwa kwenye maji ya moto kisha mgonjwa kuyanywa maji hayo, husaidia kuondoa sukari chafu na sumu kwenye damu.

Mwarobaini pia hupanua mishipa ya damu, hunaboresha mzunguko wa damu na mizani ya viwango vya kusukuma moyo.
Shinikizo la Damu:
Hurejesha mapigo ya moyo yasiyokuwa ya kawaida katika hali inayofaa na kupunguza shinikizo la damu.
Aidha, kupitia utafiti uliofanywa na Wataalam unaonesha kuwa, ikiwa mgonjwa atadungwa sidano yenye majimaji ya majani ya mwarobaini, basi kutamwezesha kupunguza shinikizo lake la damu.

Kuuwa wadudu:
Chukua mbegu chache, weka maji, ponda kisha chuja kwa chujio safi, kisha tumia maji hayo kupulizia mazao yako shambani au nyumbani kwa wadudu watambao mfano sisimizi nk.
Uzazi wa mpango:
Mwarobaini ni dawa ya asilia ya uzazi wa mpango kwani huzuia utengenezaji wa seli za manii bila kuathiri uzalishaji wa homoni.
Inaaminika kuwa, ni dawa bora ya kuchangia uzazi wa mpango kwani ni ya asili, inapatikana rahisi, haina sumu na bei yake ni rahisi kwa karibu kila mtu.

Mafuta yatokanayo na mti huu yanaweza kutumika kama dawa ya kuua mbegu. Wqnadai unapaka ukeni (kwa njia ya ndani) kabla ya tendo la ndoa na hapo itauwa manii na kuzuia ujauzito.
Saratani:
Wanasema, Majani ya mwarobaini yana uwezo mkubwa katika kuzuia uharibufu wa seli (antioxidants), halafu husaidia kuzuia saratani na pia katika kupambana na maambukizi ya saratani mwilini.
Mmeng’enyo wa Chakula:
Kunywa maji ya majani ya mwarobaini au magome, ili kutibu shida za kumengenya chakula.

Homa:
Majani ya mwarobaini ni tiba tosha kwa homa ya matumbo na Malaria, usafishaji damu, ambapk pia husaidi mzunguko na uboreshaji wakati wa hedhi.
Tiba ya Ngozi:
Matumizi ya kawaida ya mchanganyiko wa majani ya mwarobaini hasa kwa kuongezea manjano na Matango hufanya matokeo wa ngozi yako kuwa bora zaidi.
Ikiwa mchanganyiko huu utatumika usoni wakati wa kwenda kulala usiku, basi unaambiwa wale dada zetu wanaweza kuzifanya ngozi zao kuwa nyeupe zaidi.

Vidonda, chunusi:
Mchanganyiko wa majani ya mwarobaini na manjano ni bora hapa Maambukizi ya magonjwa ya ngozi kama vile vipele, ngozi kukauka nk.
Utayarishaji wake ni kuponda majani ya mwarobaini na kupaka maji yake kwenye ngozi. Aidha, inashauriwa pia kutumia majani yaliyokauka na kusagwasagwa kusugulia ngozi.
Ukichukua kiasi kidogo cha mafuta ya mbegu ya mwarobaini na kuyaweka katika maji kisha ukayaoga, husaidia kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngozi.

Nta kwenye Damu:
Chai ya Majani ya mwarobaini hupunguza nta (cholesterol) kwenye damu, lalini pia ili kuboresha Afya ya Macho inashauriwa kuosha macho na chai baridi ya majani ya Mwarobaini.
Misuli, maumivu:
Chai ya majani ya mwarobaini na maua yaliyochemshwa kwa pamoja ni dawa ya kuondoa sumu kwenye misuli,I Titi, Saratani ya kibofu na Saratani zote.
Majani ya mwarobaini huharibu mfumo, kuboresha mwitikio wa kinga, kuondoa sumu zinazoathiri seli na kuzuia athari za uchochezi. Inaharibu seli za saratani haswa ukuaji wa saratani ya kibofu na kuzuia kuenea kwake.

Kusafishaji Damu:
Majani ya mwarobaini husafisha damu na kuleta ufanisi zaidi hasa ikichanganywa na na asali.
Maumivu ya koo:
Kusukutua maji ya mwarobaini mara kadhaa kwa siku kutasiaid mno katika kuondoa maumivu ya kooni.
Mba na Nywele kudondoka:
Osha nywele mara kwa mara na chai ya majani ya mwarobaini ili kuzuia tatizo hilo.

Maumivu:
Maji ya majani ya mwarobaini na mbegu zake ni dawa nzuri ya kuzuia maumivu mbalimbali, yakiwamo ya kichwa.
Bakteria:
Majani, magome, na karibu sehemu zote za mwarobaini zina kemikali nzuri ya kuzuia athari za bakteria.
Kutibu ya nywele:
Chemsha majani machache ya mwarobaini katika maji kidogo na utumie kuosha nywele kwani Maji ya majani hayo yana antifungal, antiparasitic, antibacterial na antiviral itakayosaidia kuponya mba, shida za kudondoka nywele nk.

Majeraha ya moto:
Maji ya majani ya mwarobaini yakiachwa juu ya kidonda hufanya kazi haraka na ikumbukwe kuwa Mwarobaini pia ni muhimu katika kutibu Tetekuwanga, Mabaka meusi, na kuimarisha Afya ya Ini.
Pia Mwarobaini hutibu Ukoma, Magonjwa ya kucha, Upara, Miguu dhaifu, Maambukizi ya virusi, Kuumwa kwa meno na Matibabu ya Meno, Pumu, Makovu na Rangi Rangi, Kuumwa na wanyama na wadudu wenye sumu nk.


