Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni ndivyo tunaweza kusema msemo huo uliohasisiwa na wahenga, baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kufanikiwa kufanya upasuaji na kutoa mimba iliyokuwa imetunga nje ya kizazi na kudumu kwa miaka minne mwanamke mmoja (55), mkazi wa Shinyanga ambaye jina lake limehifadhiwa.
Kwa mujibu wa daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na uzazi wa hospiatli ya rufaa ya mkoani Shinyanga iliyopo kata ya mwawaza halimashuri ya manispaa ya Shinyanga Dkt. Augustino Maufi amesema ujauzito huo ulikuwa na uzito wa kilogram 1.6 na baada ya kufanyiwa upasuaji kiumbe kilichokuwa ndani ya ujauzito huo kilikutwa kimefariki.

Akizungumzia tatizo hilo mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji huo amesema alikuwa akienda kwa waganga wa tiba za asili kwa ajili ya kumaliza changamoto hiyo iliyokuwa ikimkabili kwani alikuwa akisikia maumivu makali ya tumbo na kukoma kwa hedhi kwa kipindi kirefu lakini baadae mganga aliyekuwa akimtibia alifariki dunia nay eye kulazimika kwenda hospitali
Katika hatua nyingine Dkt. Maufi ametoa wito kwa wale wote waganga wote waoshugulika na tiba za asili kuhakikisha wanawashuri wagonjwa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu Zaidi pindi inapotokea wameshindwa kuwasaidia ili kuweza kuokoa maisha yao.
