MAAFISA USTAWI WA JAMII SHINYANGA WAJENGEWA UWEZO UTOAJI HUDUMA KWA KUFUATA MIONGOZO, MIIKO YA KAZI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Maafisa Usitawi wa Jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,Hospiitali ya Rufaa ya Mkoa na Makazi ya Wazee Kolandoto wamejengewa uwezo kuhusu miongozo, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mafunzo hayo yamewahusisha  pia  maafisa waliojairiwa kwa mkataba na  maafisa wapya waliopangiwa katika vituo mbalimbali vya huduma, ikiwemo vituo vya kutolea huduma za afya, ngazi ya Wilaya na kwenye  makazi ya wazee Kolandoto mkoani humo.

Akifungua kikao kazi hicho, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa,  Timothy Sosoma, amewatka  washiriki kuzingatia miongozo na maadili ya kazi wanapotekeleza majukumu yao, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na kubadilishana uzoefu ili kuboresha huduma.

Ameeleza  kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi zao na kufahamiana.

“Mafunzo haya mkiyatumia ipasavyo yatawasaidia kutekeleza majukumu yenu kwa ubora unaohitajika, mkizingatia miongozo, maadili na ushirikiano katika kazi,” alisema Sosoma.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga,  Lydia Kwesigabo, amewasisitiza  washiriki kuzingatia maadili ya taaluma ikiwemo kuzingatia  faragha na kutunza siri za wateja, kutohukumu mtu kutokuwa na ubaguzi,kujipambanua na kufanya kazi kwa uadilifu.

Katika mafunzo hayo, washiriki wamejengewa  uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo huduma za ustawi wa jamii, miiko katika utoaji huduma,kujijali pamoja na mwongozo wa utoaji huduma katika makazi ya wazee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *