Maafisa 62 wamehitimu Shahada ya Sayansi

Maafisa 62 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Novemba 18, 2023 wamehitimu Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na kutunukiwa Kamisheni na Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha.

Hii ni mara ya kwanza kwa chuo hicho kuwezesha mafunzo ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi kwa kujisimamia chenyewe pasipo na ushirikiano wa kimafunzo na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kama ilivyokuwa kwenye awamu 3 zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *