MAADHIMISHO YA NNE YA LUGHA YA KISWAHILI YAPOKELEWA KIPEKEE ZIMBABWE

Maadhimisho ya nne ya Lugha ya Kiswahili, yamefanyika Zimbabwe huku yakipokelewa kwa namna ya kipekee na washiriki kutoka maitafa mbalimbali.

Maadhimisho hayo, yaliyofanyika Julai 11, 2025 katika Ukumbi wa Museum of Africa Liberation, Heritage Village yakilenga kuendeleza na kukuza lugha hiyo, ili kuleta mshikamano na maitaifa mengine duniani.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya Elimu ya Juu wa Zimbabwe, Balozi Frederick Shava, ambaye alisisitiza kuwa yanapaswa kuenziwa kwa lengo la kuleta umoja wa kimataifa na maendeleo ya lugha ya kiswahili.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Kiswahili kwa Amani na Mshikamano” ambapo Balozi Shava ameweka wazi kuwa inaakisi dunia ya leo huku amewaomba washiriki wa maadhimisho hayo kuendelea kujifunza na kukielewa kiswahili.

Naye Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda amesema kuwa lugha ya kiswahili ni tunu, daraja na nyenzo muhimu katika kukuza maendeleo na kudumisha mshikamano.

Amesema, lugha ya Kiswahili ni kiungo kilichotumika katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika “pale Tanzania ilipokuwa mwenyeji wa Wapigania uhuru kutoka Vyama vya Ukombozi vikiwemo ZANU PF, FRELIMO, SWAPO, ANC.”

Maadhimisho hayo, yamehudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo walitoa Salaam za pongezi kwa mshikamano huo ambao ulitolewa na Nisha, Mwakilishi wa UNESCO nchini Zimbabwe, Nisha na Balozi wa Kenya nchini Zimbabwe, Gertrude Angote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *