Maadhimisho ya kupiga vita dawa za kulevya ni muhimu

Imeelezwa kuwa Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi na Biashara ya Dawa za kulevya Duniani ni muhimu kwani yamekuwa yakitumiwa na Serikali kuonesha nia yake ya kushirikiana na Jumuia za kimataifa na jamii katika mapambo dhidi ya Dawa za kulevya.

Hayo yameelezwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas James Lyimo katika kilele cha maadhimisho hayo Mkoani Arusha.

Katika kilele cha maadhimisho hayo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *