Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Lupita Nyong’o apata penzi jipya?

Waswahili wanasena wape picha stori wanayo!! Mwanadada ambaye ni muigizaji wa filamu kutoka Hollywood Lupita Nyong’o amenaswa na mapaparazi akiwa na Mwigizaji wa filamu kutoka Canada, Joshua Jackson.

Wawili hao wamenaswa wakiwa matembezini na wapo kwenye mapozi ya kimahaba, Utakumbuka Oktoba 20 mrembo huyo aliweka wazi kuachana na mpenzi wake Selema Masekela kwa kile alichodai kufanyiwa unyanyasaji wa kimwili.

Na Oktoba mwaka huu Joshua na Lupita walinaswa pamoja kwenye tamasha la muziki mjini Los Angeles. Wakati huo pia Joshua alikuwa ametalakiana na mkewe Jodie Turner-Smith, huku mkewe akidai kuwa ndoa yao imekuwa sio ya furaha, lich aya kubarikiwa kupata watoto wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *