
Mahakama ya Katiba ya Nchini Zambia imesema kuwa Rais wa zamani Edgar Lungu hapaswi kugombea tena Urais muhula mwingine kwenye uchaguzi wa mwaka 2026 kwa sababu tayari amehudumu kwa mihula miwil.
Uamuzi huo unajumuisha kipindi cha Lungu kama rais kati ya 2015 na 2016 baada ya Michael Sata kufariki akiwa madarakani kilihesabiwa kama muhula kamili. Baadaye Lungu alishinda uchaguzi kwa muhula wa pili kutoka 2016 hadi 2021.

Lungu alitangaza kurejea katika siasa mwaka jana na alilenga kumkabili Rais wa sasa Hakainde Hichilema katika uchaguzi mkuu ujao, Maamuzi ya mahakama hiyo ya Zambia yalitangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa na redio.
Zambia ni lililoko kusini mwa Afrika lenye takriban watu milioni 20 na ni miongoni mwa wazalishaji 10 wakuu wa madini ya shaba duniani.