Shabiki, aliyepata umaarufu mkubwa wakati wa fainali za AFCON 2025 nchini Morocco, Michel Kuka Mboladinga (Lumumba Vea), hatohudhuria mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, baada ya kukosa viza ya kusafi kwenda Mexico.

Hata hivyo, Lumumba huyo bado ana nafasi ya kupata viza nyingine kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia, iwapo DRC itafuzu na tayari amewataarifu mashabiki wake kilichojiri.