
Staa wa muziki Loui, amemrarua CEO wa Konde Gang, Harmonize kwa kile ambacho amekisema jana juu ya kupewa heshima kwa kufanya muziki wa Bongo Flava kwa lugha ya Kiingereza.
Kupitia Instastory yake Loui amesema kuwa yeye ndio msanii wa kwanza kufanya ngoma (Hennessy) ambayo walitumia lugha Kiingereza na kufanya ngoma hiyo kupenya ulimwenguni, wakati huo huo kumeikuba habari kuwa Harmonzie aliichingia baharini video ya Loui na kumsababishia hasara ya Milioni 18, hali iliyopelekea msanii huyo kukaa kimya kwa muda mrefu.

