Gari aina ya scania lenye usajili wa namba T124 ECX linalobeba sumu ya Sodium Cyanide inayapeleka Migodini mitatu nchini limepata ajali eneo la Kagongwa na sumu hiyo kumwagika.
Akizungumza leo Oktoba 17 Wilaya ya Kahama baada ya kufika kwenye tukio Kamanda wa Mkuu wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Janeth Magomi amesema alipata taarifa majira ya saa 3:20 asubuhi gari la Kampuni ya Taifa Transport & Logistic limedondoka katika Kata ya Kagongwa Wilaya ya hiyo kwenda eneo tukio.
Amesema vyombo vya usalama vinaendelea na udhibiti kuepusha madhara kwa wananchi lazima tahadhari ziwepo kwa sababu sumu ni hatari.
“Nilivyofika kwenye eneo la tukio ni kweli ajali imetokeoa na huduma za uokaji zinaendelea ambapo dereva mmoja kati ya madereva kumi waliokuwa wakisafirisha sumu ya Sodium Cyanide amepata ajali na kapewa huduma na kuhakikisha madhara hayotokei kwa wananchi, ” amesema Kamanda Magomi.
Pia amesema dereva huyo amepewa huduma ya kwanza kutoka kwa waaguzi na anaendelea vizuri na hali ni shwari kwa wananchi wote wa eneo hilo na kuwataka waaendelee na shughuli zao za kila siku na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Naye, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mkaguzi wa Wilaya ya Kahama, Edward Selemani amesema wao wamejianda kufanya uokaji muda wowote tukio linapotokea.