Uongozi wa klabu ya LIPULI FC inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania bara (First League) msimu wa 2023/24, umetangaza kuitoa timu yao kwenye ligi hiyo, kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha unaoikabili huku wachezaji wake wakikosa leseni ya kucheza ligi.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Shukuru Luhambati, amesema kama uongozi walifanya juhudi kubwa binafsi kuisaidia timu hiyo lakini wameshindwa huku wakikosa sapoti ya serikali ya mkoa ambayo iliahidi kuisaidia timu hiyo na Ruvu Shooting iliyonunuliwa na serikali ya mkoa wa Iringa.
Amesema tayari wameshaandika barua bodi ya ligi ya kujitoa kwenye ligi daraja la pili Tanzania bara msimu huu.
Hadi sasa timu hiyo haikuwa na alama hata moja, na kwa mujibu wa adhabu zilizotolewa na bodi ya ligi kwa awamu mbili timu hiyo jumala imekatwa alama 30 na faini ya shilingi milioni 6.