Kwa sasa kasi ya Internet ni Mara 10

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, @napennauye amesema Mkongo wa bahari uliozinduliwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan utasaidia kuongeza kasi ya intaneti iliyopo mara 10 zaidi.

Nape ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 10, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa baharini.

“Mkongo utaongeza kasi ya mtandao wa intaneti zaidi ya mara 10 ya sasa, ubora wa intaneti utaongezeka, utashusha gharama za mtandao huo hapa nchini na ni fursa kubwa ya kuvutia uwekezaji wa kampuni kubwa kama vile Guco, Meta na Netflix ambapo pamoja na kukuza uchumi wetu, itatoa ajira kwa vijana,” amesema.

Aidha, Nape ameongeza kuwa mkongo wa baharini wa “To Africa” ndiyo mkongo mrefu zaidi duniani, kwa hiyo hapa wamefanya jambo kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *