KUWASA KAHAMA YAANZA KUWAUNGANISHIA MAJI WATEJA WALIOLIPIA MUDA MREFU

William Bundala, Kahama – Shinyanga.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), imeanza kuwaungaishia maji wananchi ambao walifanya malipo muda mrefu ili kuunganishiwa huduma hiyo.

Hayo yamebainishwa na Afisa uhusiano wa mamlaka hiyo John Mkama wakati akizungumza na Jambo Fm Kuhusu hatua za kuwaunganishia huduma yam aji wananchi ambao wamelipia muda mrefu.

“Tulikuwa na changamoto ya vifaa,wateja wetu waliiomba huduma tangu mwezi wa tatu na wamelipia wamechelewa sana kupata huduma ya maji,maana mzabuni wetu ambaye anatusambazia vifaa akawa anapata vifaa nusunusa ila jitihada zimefanyika vifaa vimekuja na tumeenza kuwaunganishia wateja wetu tangu mwishoni mwa mwezi wa sita” Amesema Mkama.

Sambamba na hayo Mkama amesema kuwa mfumo wanautumia kuwaunganishia maji ni kuanza na wale ambao walilipia mapema kisha na wengine waliolipia sasa watafuata.

“Na mfumo tunaotumia tunatumia mfumo wa aliyelipa wa kwanza ndiye anatoka wa kwanza,yani wale watu waliolipa mwanzoni ndio wanapata kwanza alafu wale wengine waliolipa nyuma wanafuata,tunafanya hivi ili kuondoa malalamiko kwa wateja wetu” Ameongezea Mkama.

Nao baadhi ya wananchi waliopata vifaa vya kuunganishiwa maji William Gabriel na Asia Amocy wameshukuru kwa kuanza zoezi hilo na kuiomba maamlaka ikomeshe wizi wa dira za maji ambao umekithiri Kahama.

“Tunashukuru kwa kupata vifaa mana tulilipia muda mrefu sana lakini ombi langu kwa Kuwasa wakomeshe wizi wa Dira za maji yani kwa manispaa ya Kahama umekithiri sana,Kwa kweli wizi ni mkubwa na wasipokomesha wizi huu hata hivi vifaa tulivyopokea leo vitaibiwa tena” Wamesema William Gabriel na Asia Amocy akazi wa mtaa wa Majengo Kahama.

Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama ilianzishwa tarehe 21 Juni 2002 kwa sheria ya “water works Act cap 272” iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009 na inapokea maji kutoka chanzo cha  Ziwa Victoria ambako maji yanasafirishwa kwa umbali wa kilomita 117 kwa njia ya mabomba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *