Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kuwa dereva wa Serikali haina maana uko juu ya sheria

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka madereva wa Serikali kuwa mfano wa kuzingatia sheria zote kwa sababu kuendesha gari ya Serikali haimaanishi wamepewa rungu la kuvunja sheria bali wanapaswa kuwa mfano wa kuzizingatia hasa zile za usalama barabarani.

Majaliwa amesema kuwa, “ukiwa dereva wa Serikali haimaanishi kuwa uko juu ya sheria bali kila dereva anatakiwa kuwa mfano wa kuzingatia sheria zote. Aidha, madereva wa vyombo visivyo vya Serikali wanapaswa kujifunza kutoka kwenu madereva wa Serikali.”

Pia, Waziri Mkuu amesema madereva hao wanapaswa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya taaluma ya madereva wa Serikali ambayo yanawataka madereva hao kuzingatia na kutii sheria za usalama barabarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *