Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kutorosha madini sio uzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan amezindua na kukabidhi vitendea kazi ikiwemo mitambo ya uchorongaji, mitambo ya kuzalisha nishati mbadala, magari na mtambo wa kusaga kokoto kwa Wachimbaji wadogo wa Madini Leo Oktoba 21,2023.

Vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la Madini STAMICO chini ya Wizara ya Madini katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma, ambapo ametoa wito kwa wachimbaji wadogo kuuza madini Yao katika viwanda vya ndani na Kuacha tabia ya kutorosha madini kwani huo sio uzalendo.

Aidha Rais ametoa wito Taasisi za kifedha kuwaamini wachimbaji wadogo na kuwapa mitaji ili waweze kuzalisha kwa wingi na kukuza uchumi wa wachimbaji wadogo na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Rais Samia amemshukuru na kumpongeza Dkt. Biteko kwa kazi kubwa aliyoifanya katika Sekta ya Madini kabla ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambapo amesema kuwa ametekeleza maelekezo aliyompa wakati akimuapisha kuwa Waziri wa Madini ambapo alimtaka kuhakikisha sekta ya madini kufikia mwaka 2025 inachangia asilimia 10 katika pato la Taifa jambo ambalo alilifanikisha mapema kabla ya muda aliopewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *