KUPPET WALAANI MWALIMU KULAZWA KWA KIPIGO AKIDAIWA KUCHELEWA SHULENI

Maafisa wa Muungano wa Walimu wa Elimu ya Sekondari Kenya (KUPPET), wamelaani shambulio la Mkuu Nyanchoka wa Shule ya upili iliyopo eneo la Ikonge, dhidi ya Mwalimu Vicent Onyancha na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Mwl. Onyancha alikumbwa na mkasa huo wakati akifundisha darasani ambapo amedai Mkuu wake alimvamia na kuanza kumpiga na kumzaba makofi yaliyopelekea kupata majeraha na kulazwa katika Hospitali ya Ikonge.

Mwalimu Vicent Onyancha akiwa amelazwa katika Hospitali ya Ikonge. (Picha ya Citizen Digital).

Akisimulia tukio hilo, Mwl. Vicent anasema, ” alinipiga teke na kofi. Kisha akaniburuta hadi ofisini kwake ambako aliendelea kunishambulia akidai nilichelewa kufika Shuleni.”

Hata hivyo, Viongozi hao wa KUPPET walionya kwamba, Walimu wataingia katika mgomo, iwapo hakuna hatua zitakazochukuliwa na mamlaka husika dhidi ya Mkuu wa Shule hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *