Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kulala mchana kuna faida zake

Linapokuja sula la usingizi basi huwezi kukwepa kabisa,  Na ndio maana tunashauriwa upate japo dakika chache mchana ulale ili uwe sawa. Ila katika jamii zetu kulala mchana inaweza kuonekana kama uvivu. Yaani mtu anayelala mchana anaonekana ni mvivu na hapendi kazi.

Ila kulala mchana kuna faida kubwa sana kuliko ulivyowahi kufikiri. Na leo tutapata kuzijua faida chache za kulala mchana na kama utaweza uweke ratiba hiyo kwenye kila siku yako.

1. Inapunguza stress.

Kufanya kazi kwa siku nzima inaweza kukufanya uwe na stress nyingi sana. Kupata dakika chache za kulala inapunguza stress hizi.

2. Inaongeza uwezo wa kujifunza na kumbukumbu.

Ni rahisi sana kujifunza na kukumbuka yale uliyojifunza kama akili inakuwa imepumzishwa. Kulala mchana kunaipumzisha akili.

3. Inaongeza ubunifu.

Kama unafanya kazi ambazo zinahitaji ubunifu wa hali ya juu kuwa na utaratibu wa kulala mchana na unapoamka unakuwa katika nafasi nzuri ya ubunifu.

4.  Ni bora kwa afya yako.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wanaolala mchana wanauwezekano mdogo wa kupata magonjwa ya moyo ukilinganisha na ambao hawalali mchana.

5. Inaongeza ufanisi.

Watu ambao wanalala mchana huamka wakiwa na ufanisi mkubwa kuliko ambao wanafanya kazi siku nzima.

Zingtia kulala mchana ni kati ya dakika 20 mpaka 25. Hivyo hata kama unafanya kazi unaweza kutenga dakika 20 baada ya chakula na ukasinzia au kulala kidogo. Sio lazima ulale kitandani, hata kkuinamisha kichwa chako kwenye meza inakutosha kunufaika na usingizi huo.

Haya yamebainishwa na  Dr. Makirita Amani katika Makala yake ya mwaka 2014.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *