Kujiunga JKT ni Bure

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ametangaza nafasi za Kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka wa 2023 kwa Vijana wote wa Kitanzania waliomaliza darasa la Saba mpaka chuo kikuu.

Akitoa taarifa hiyo leo Agosti 25, 2023 Jijini Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema kuwa utartibu wa Vijana kuomba nafasi hiyo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na Wilaya.

Aidha Brigedia Jenerali Mabena amesema nafasi hizo zinatolewa Bure hakuna malipo yoyote yatakayoambatana na nafasi hizo au kutafutiwa ajira mara baada ya kumaliza mafunzo ya JKT.

Usaili utaanza agosti 28, 2023 kwa mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na Vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye kambi za JKT kuanzia Septemba 26 hadi Septemba 29, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *