Kuiba mitihani ni kujenga jamii isiyo na maadili

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) lilianzisha kampeni ya kupambana na wizi wa mitihani si kwa sababu wizi huo umekithiri nchini, bali ni kutatua wizi uliokuwa ukijitokeza mara chache.

Profesa Mkenda amesema hayo Mkoani Dar es Salaam wakati wa kufungua maonesho ya NECTA, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo.

Ameongeza kuwa kuiba mitihani si uadilifu, kwani kufundisha Wanafunzi wizi ili kufanikisha kuiba mitihani ni kujenga jamii isiyo na maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *