Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa taarifa kwa umma kuhusiana na ajali iliyotokea siku ya Jumamosi tarehe 4 Januari, 2025 majira ya saa 8:45 mchana, iliyohusisha Gari ya kampuni ya Wakali Safaris yenye namba za usajili T450 APB.
Ngorongoro wamesema ‘Ajali hii imetokea kati ya Viewpoint na lango kuu la Loduare ambapo gari hilo lilikuwa na watu saba, kati ya hao watu sita ni raia wa Israel na mtu mmoja ni Mtanzania ambaye ni dereva wa kampuni ya Wakali Safaris. Baada ya ajali hiyo kutokea watu wote waliokolewa na majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika hospitali za Lutherani na FAME zilizopo wilaya ya Karatu kwa huduma ya kwanza na baadaye kusafirishwa kwenda hospitali ya Lutherani ya Selian jijini Arusha kwa matibabu zaidi’ – Ngorongoro.
‘Ajali hiyo imesababisha majeruhi watano (05) na mtu mmoja (01) mwanamke amefariki dunia. Hali ya dereva ni mima na anaendelea vizuri. NCAA inaendeela kuwakumbusha madereva wote wa gari za watalii kuzingatia sheria za barabarani na sheria za Hifadhi ili kuendelea kuwa salama kwa wageni na vyombo wanavyotumia wakati wote wanapokuwa hifadhini’ – Ngorongoro
‘Mamlaka itaendelea kutoa taarifa kadri inavyowezekana. Tunaomba Mungu awawezeshe majeruhi apone haraka na marehemu apumzike kwa amani. Amina!’ – Ngorongoro