KUCHAPISHA PICHA YA MTOTO MAZINGIRA HATARISHI NI KOSA KISHERIA, KUNA JELA NA FAINI

Na Irene Kishiwa – Chumba cha Habari.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na watengeneza maudhui mtandaoni, ambao wanachapisha picha na kutoa maudhui ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kuacha kufanya hivyo, kwani ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Kifungu cha 162 kifungu kidogo cha (1) K kinaeleza kuwa ni makosa kutengeneza, kusambaza ama kumuwezesha mtu mwingine kusambaza picha za watoto ambao wako kwenye mazingira hayo.

Kamishna Msaidizi Huduma ya Ustawi wa Jamii na Watoto Kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Happy Msimbe amesema sheria imetengeneza adhabu zake kwa mtu yeyote atakae husika kutengeneza na kusambaza maudhui ya namna hiyo, na kwamba adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni tano, kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Amesema, “Mtoto huyu si kwamba anaishi katika maeneo hayo kwa kupenda bali huwenda kuna changamoto flani ambazo zimemlazimisha kuishi hapo mtoto huyu huwenda angekuwa kiongozi wa baadae katika familia na Taifa na wakati mwingine anatamani kuyafuta nakusahau makovu anayopitia kutokana na machapisho hayo makovu hayo yawezi kufuta kumbukumbu hizo.”

Licha ya utengenezaji wa maudhui ya namna hiyo Mitandaoni, bado ni njia mojawapo ama kuwa chanzo cha ajira kwa baadhi ya watu, kutokana na kuchapisha picha mjongeo au mnato za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, na kuzitumia katika mitandao hiyo, bila kujua kuwa ni kosa kisheria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *