Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limezuia jaribio la mapinduzi lililohusisha wapiganaji raia wa Kongo na wa kigeni mapema leo asubuhi.
Msemaji wa jeshi hilo Sylvain Ekenge ameyasema hayo katika hotuba yake kupitia televisheni ya taifa hilo na kueleza kwamba Jaribio la kuipindua serikali lililofanywa na waakongo walioshirikian na raia wa kigeni na kueleza kwamba watu hao hawakupata nafas I ya kusanbabisha madhara lakini hajaweka wazi iwapo watu hao walikamatwa au kuuawa.
Mapema leo, watu watatu wakiwemo walinzi wawili na mshambuliaji mmoja waliuawa katika shambulio kwenye makazi ya mwanasiasa Vital Kamerhe, mbunge anayewania kiti cha spika wa bunge la taifa hilo, mapigano yaliripotiwa kati ya watu wenye silaha waliovalia sare za jeshi na walinzi wa mwanasiasa huyo kwenye makazi katika eneo la Tshatshi Boulevard, takriban kilomita mbili karibu na Ikulu ya nchi hiyo na baadhi ya ofisi za balozi za kigeni.
Msemaji wa Vital Kamerhe, Michel Moto Muhim, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kuwa, mwanasiasa huyo na familia yake wako salama na kwamba ulinzi wao hivi sasa umeimarishwa.
Mwanasiasa wa Kongo DRC Vital Kamerhe aliyenusurika katika tukio la watu watatu wakiwemo walinzi wake wawili na mshambuliaji mmoja kuuawa katika shambulio lililofanyika kwenye makazi yake.
Jaribio hilo la mapinduzi linatokea katikati ya mivutano ndani ya chama tawala cha Rais Felix Tshisekedi juu ya nafasi ya kiti cha spika wa bunge la taifa katika uchaguzi uliopangwa kufanyika jana Jumamosi na ambao umeahirishwa na vyombo vya habari ndani ya Kongo vimesema waliohusika na shambulio hilo ni wanajeshi wa Kongo.
Ijumaa ya Mei 17, Rais Felix Tshisekedi alikutana na wabunge na viongozi wa chama tawala katika jaribio la kuutatua mzozo ndani ya chama hicho na alikwenda mbali zaidi na kutishia kulivunja bunge na kumrudisha kila mtu nyumbani kwenye uchaguzi mpya iwapo kile alichokiita mazoea mabaya yataendelea.
Ubalozi wa Marekani nchini Kongo ulitoa tahadhari ya usalama na kuwahimiza watu kuwa macho kufuatia ripoti za kutokea makabiliano ya risasi.