Kofia ambayo aliivaa nguli wa pop Michael Jackson, kabla ya kutumbuiza kwenye shoo yake ya kwanza ya ‘Moonwalk’ mwaka 1988 imeuzwa huko mjini Paris kwa kiasi cha $82,170 sawa na Milioni 200 za Kitanzania.

Kofia hiyo nyeusi aina ya Fedora, ilikuwa ni miongoni mwa vivutio 200 zilivyokuwepo kwenye mdana huo ambapo umefanyika wiki kadhaa kwenye Hoteli ya Drouot.



