
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Morocco, AS Far Rabat inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Mohamed Nasreddine Nabi, imetenga ofa nono kuinasa saini ya mlinzi tegemeo wa Simba SC, Hennock Inonga Baka.
Mchezaji huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Simba SC. Miamba hiyo tayari imewasilisha ofa yao mezani kwa Simba SC kuona uwezekano wa kumnasa.
Inakisiwa kuwa, Simba SC inaweza kuwa tayari kumuachia mlinzi huyo, iwapo kiasi cha dola za Marekani zaidi ya 500,000 (Bilioni 1.2) kitatolewa na Vinara hao wa ligi ya Morocco.