Kocha na Golikipa wafariki kwenye ajali

Shirikisho la soka nchini Algeria, limesema ajali ya basi lililopinduka imeua washiriki wawili wa ligi kuu nchini humo (Ligue 1) wa klabu ya MC El Bayadh na hivyo shirikisho hilo litahairisha mechi zote za wiki hii.

Shirikisho hilo limesema waliofariki katika ajali hiyo ni golikipa wa akiba wa timu hiyo Zakaria Bouziani (27), na kocha msaidizi Khalid Muftah. Bouziani amedaka mechi mbili za ligi msimu huu.

Vyombo vya habari vya Algeria vimesema, basi hilo limepinduka katika mji wa Sougueur kaskazini magharibi mwa Algeria, lilipokuwa njiani kuelekea mjini Tizi Ouzou kucheza mechi ya ligi dhidi ya JS Kabylie Ijumaa hii.

MC El Bayadh imesema kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa, waliojeruhiwa wanaendelea vizuri. Huku ikielezwa kuwa dereva wa basi hilo nae amefariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *