Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kocha Geita Gold atakiwa kujisalimisha

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi amemtaka kocha mkuu wa timu ya Geita Gold inayomilikiwa na Halmashauri hiyo afike ofisini kwake mara moja kueleza kiini cha matokeo mabaya.

Zahara ametoa maelekezo hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari mjini Geita na kueleza haridhishwi na mwenendo wa timu hivo benchi la ufundi wafike kumueleza kikwazo ni nini.

Amekiri matokeo ya suluhu waliyopata Geita Gold Fc ugenini mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons yanatoa mwanga wa mabadiliko lakini lazima hatua thabiti zichukuliwe kumaliza ukata wa matokeo mazuri.

Zahara amesisiza timu ya Geita Gold mpaka sasa ipo kwenye matazamio na yeyeote atakayesumbua na kuonekana kikwazo ndani ya timu atachukuliwa hatua kulingana na makubaliano ya mikataba.

Ikumbukwe Geita Gold Fc inafundishwa na kocha Hemed Suleiman, ambaye tangu apewe dhamana hiyo, imecheza michezo nane ya ligi kuu ya Tanzania bara na kupoteza michezo minne, kupata sare tatu na ushindi mmoja pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *