
Aliyekua kocha wa timu ya Yanga, Miguel Gamondi leo Julai 03 2025 ametambulishwa rasmi na klabu ya Singida Big Stars kama kocha mpya wa timu hiyo yenye maskani yake Mkoani Singida.

Kupitia kurasa zao za Mitandao ya Kijamii Singida Black Stars wameandika ‘TAARIFA KWA UMMA’
‘Tunayo furaha kumtambulisha MIGUEL GAMONDI kuwa Kocha Mkuu wa timu yetu kwa mkataba wa mwaka mmoja. Wakati huo huo, Kocha David Ouma na Kocha Moussa N’Daw watakuwa Makocha Wasaidizi.’

‘Mabadiliko haya katika Benchi la Ufundi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026.’ – Singida Black Stars